TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 30.09.2022

Juao Cancelo
Beki wa Manchester City Juao Cancelo

Real Madrid watajaribu kumsajili beki wa Manchester City na Ureno Joao Cancelo, 28, msimu ujao wa joto na pia wanapanga kumnunua mshambuliaji wa City wa Norway Erling Haaland mwenye umri wa miaka 22 mwaka wa 2024. (AS - kwa Kihispania).

Kiungo wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, anaonekana na Barcelona kama shabaha ya muda mrefu kuchukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Sergio Busquets, 34. (Sport).

Newcastle United imewajumuisha kiungo wa kati wa Leicester City na Uingereza James Maddison, 25, na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, katika malengo yao kwa 2023. (90 min).

ruben neves
Kiungo wa Wolves Ruben Neves

Timu inayojumuisha nyota wote Ligi ya Primia inaweza kucheza na timu za ligi pinzani kama vile La Liga au Bundesliga chini ya mipango inayozingatiwa na wakuu wa vilabu. (Times - usajili unahitajika)

Aston Villa hawana nia ya kumruhusu mlinda mlango wa Argentina Emiliano Martinez, 30, kuondoka mwezi Januari huku Manchester United ikiwa miongoni mwa klabu zinazomwania. (Football Insider)

Klabu za Manchester United, Southampton na Everton bado zinamwania mshambuliaji wa PSV Eindhoven na Uholanzi Cody Gakpo, 23, na wanaweza kuhama wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Football Transfer)

Emiliano Martinez
Goli kipa wa Argentina Emiliano Martinez

Brighton wanapanga kufanya mazungumzo ya kandarasi na mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard, 27, na kiungo wa kati wa Argentina Alexis Mac Allister, 23. (Athletic - usajili unahitajika)

Liverpool wanafikiria kumnunua winga wa Misri na Pyramids Ibrahim Adel Januari huku Arsenal, Brentford, Brighton na Nottingham Forest pia wakiwa katika msururu wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (90 Minutes)

Mkufunzi wa Tottenham Muitaliano Antonio Conte, 53, amepuuzilia mbali tetesi zinazomhusisha na kurejea Juventus kuwa "zisizo na msingi" na kusisitiza kuwa ana anadhika sana Spurs. (Evening Standard)

Antonio Conte
Kocha Wa Tottenham Antonio Conte

Juventus wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal, Liverpool, Tottenham, AC Milan na Barcelona kuwania saini ya mshambuliaji wa Uhispania Marco Asensio baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kukataa kuongezewa mkataba na Real Madrid. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Chapisha Maoni

0 Maoni