TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne Septemba 20, 2022


Meneja wa Chelsea Graham Potter anataka kumnunua nyota wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 29, na badala yake yuko tayari kumpeana mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29,. (Calciomercato - in Italian).

 Liverpool wanavutiwa na winga wa Shakhtar Donetsk Mykhaylo Mudryk, 21, ambaye amefananishwa na Neymar. (Calciomercato - in Italian).

 Leicester hawawezi kumfuta kazi meneja Brendan Rodgers kwani itawagharimu pauni milioni 10 kumlipa. (Sun).

 Iwapo Leicester itamfuta kazi Rodgers, orodha yao itakayoshirikisha meneja mpya ni pamoja na Mauricio Pochettino, Rafael Benitez na Sean Dyche. (Sun)


Liverpool wanamfuatilia kiungo wa kati wa Flamengo Joao Gomes, 21, huku Jurgen Klopp akitafuta msaada katika eneo lenye tatizo. (Talksport).

 Beki wa Ufaransa Benjamin Pavard anafikiria kuondoka Bayern Munich msimu huu wa joto, huku Manchester United, Chelsea, Paris St-Germain, Atletico Madrid na Juventus zikitaka kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Telefoot, via Standard)

 Wakuu wa Manchester United wamegawanyika katika sera ya uhamisho - Erik ten Hag anataka kufanya usajili zaidi mwezi Januari, lakini mtendaji mkuu Richard Arnold anataka kusubiri hadi majira ya joto. (The Athletic)

 Vilabu vya Premier League vinaripotiwa kumchunguza winga wa Eintracht Frankfurt Ansgar Knauff, 20, huku akifananishwa na Arjen Robben (Sport1)


West Ham wamemwambia winga wa Argentina Manuel Lanzini, 29, yuko huru kuondoka mwezi Januari, na kujaribu kutafuta mnunuzi kabla ya tarehe ya mwisho ya kuhamia majira ya kiangazi. (Football Insider)

Barcelona wana nia ya kumsajili winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 26, kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Mchezaji wa kimataifa wa Uruguay Luis Suarez atatumia msimu mmoja pekee nchini kwao na klabu ya Nacional, huku rais wa klabu hiyo akithibitisha kuwa mshambuliaji huyo, 35, ataondoka mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)

Bayern Munich wamemuunga mkono hadharani meneja Julian Nagelsmann licha ya kushindwa na Augsburg wikendi na kuwaacha mabingwa hao katika nafasi ya tano kwenye ligi ya Bundesliga. (Sky Sports)



Chapisha Maoni

0 Maoni