TANGAZA HAPA

Tetesi za soka Ulaya Jumapili 25.05.2022

Klabu ya Manchester United itamuongezea mshambuliaji wake raia  wa England mwaka mmoja wa kuichezea klabu hiyo kulingana na masharti ya mkataba wake endapo pande hizo mbili zitashindwa kufikia muafaka wa mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa Rashford mwenye miaka 24 unatamatika mwishoni mwa msimu huu. (Daily Star on Sunday).

United pia inatafakari uwezekano wa kumuongezea mkataba mlinda lango wao raia wa Uhispania David de Gea mpaka kufikia mwaka 2024. Mkataba wa sasa wa kipa huyo mwenye miaka 31 utafikia kikomo mwishoni mwa msimu pia. (Sunday Telegraph).


Kocha wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino yupo tayari kwa uwezekano wa kuinoa klabu ya Aston Villa ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha Steven Gerrard. (Football Insider).

Klabu ya Newcastle inatarajia kuwasilisha dau jipya la kumsajili kiungo mshambuliaji wa Leicester City, James Madison (25) katika dirisha la usajili la mwezi Januari baada ya kushindwa kumnasa mchezajji huyo kwenye dirisha la majira ya kiangazi lililofungwa hivi karibuni. (Football Insider).


Arsenal imeendelea kumfuatilia kiungo wa klabu ya Rennes Lavro Majer wakati mchezaji huyo alipokuwa akiichezea timu yake ya taifa ya Croatia siku ya Alhamisi na kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Denmark. (Sunday Mirror).

Chelsea inajipanga kulipa dau la pauni milioni 30 kumnasa kinda wa Fulham Luke Harris, 17. Mshambuliaji huyo kinda amejumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Wales kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Ubelgiji na Poland. (Sunday Mirror).

Kiungo wa Everton raia wa Brazil Allan, 31, amekubali kujiunga na klabu ya Al-Wahda iliyopo katika nchi ya Umoja wa Falme za Kiarabu. (Football Insider).


Kiungo wa Uhispania Sergio Busquets, 34, ambaye mkataba wake na Barcelona unatamatika mwishoni mwa msimu anahusishwa na kuhamia nchini Marekani japo kiungo huyo anasema bado hajafikia maamuzi kuhusu mustakabali wake. (90 Min).

Klabu ya Barcelona itafanya mazungumzo na kiungo wake Frankie de Jong, 25, mwishoni mwa msimu kuhusu madeni anayoidai klabu hiyo na kima cha mshahara kwa siku zijazo. (Que T’hi Jugues, via Sunday Mirror).


Barcelona wanatarajiwa kujaribu kuongeza mkataba wa mlinzi Hector Bellerin, 27, kwenda Zaidi ya msimu ujao jjapo mchezaji huyo anaweza kutaka kurejea katika klabu ya Real Betis ambayo aliichezea kwa mkopo msimu uliopita. (Fichajjes.net – in Spanish).

SOURCE ; BBCSWAHILI

Chapisha Maoni

0 Maoni