TANGAZA HAPA

Tetesi za soka Ulaya Jumatano 21, 2022

Nice wanatumai wanaweza kumshawishi kocha wa zamani wa Paris St-Germain na Tottenham Mauricio Pochettino kuchukua nafasi ya Lucien Favre kama meneja wa klabu hiyo ya Ligue 1. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, anasema hajutii kusalia Leicester City msimu huu wa joto licha ya kuhusishwa na uhamisho wa kujiunga na Arsenal. (Sky Sports)

Winga wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 24, amesema "amefadhaishwa" na uamuzi wa meneja wa zamani Thomas Tuchel kutomuanzisha katika mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid mnamo 2021.. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Everton na Brazil Allan, 31, ameanzisha mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Falme za Kiarabu ya Al-Wahda katika wiki mbili zijazo. (Football Insider)


Mmiliki wa Chelsea na mkurugenzi wa muda wa michezo Todd Boehly  ameshindwa kuelewa ni kwanini utawala uliopita haukumsajili Aurelien Tchouameni kabla ya kiungo huyo kujiunga na Real Madrid. (Sport - in Spanish)

Mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, anataka kusaini kandarasi mpya na timu hiyo ya Serie A licha ya kuwavutia Chelsea. (La Gazzetta Dello Sport, via Teamtalk)

Beki wa Manchester United Lisandro Martinez, 24, na beki wa kati wa Tottenham Cristian Romero, 24, wote wameachwa kwenye kikosi cha Argentina kabla ya mechi mbili za kirafiki kutokana na masuala ya visa. (Mirror)

Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester City na Ivory Coast Yaya Toure anawasaidia vijana wa chini ya miaka 21 wa Uingereza kujiandaa kwa mechi dhidi ya Italia na Ujerumani anapojaribu kukamilisha beji zake za kuwa kocha. (Mail)


Huko Leeds United, Muingereza Jamie Shackleton anatarajiwa kuondoka Elland Road msimu ujao, huku Millwall akiwa na chaguo la kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wakati mkopo wake na klabu hiyo utakapoisha. (Athletic - subscription required)

Bodi ya wakurugenzi ya Juventus itafanya mkutano siku ya Ijumaa kujadili mustakabali wa meneja Massimiliano Allegri, huku miamba hao wa Serie A wakijikuta katika nafasi ya nane kwenye jedwali kwa kushinda mara mbili pekee kati ya mechi saba.. (Calciomercato - in Italian)

Chelsea wanamlenga mtendaji mkuu wa RB Leipzig Oliver Mintzlaff kuchukua nafasi ya mkurugenzi wa ufundi Stamford Bridge. (Athletic - subscription required)

Tottenham wako kwenye mazungumzo ya kina na mtaalam wa kuajiri Jeff Vetere ili kuongoza usajili wao wa wachezaji wasizodi umri wa miaka 21. (Football Insider)

SOURCE ; BBCWAHILI

Chapisha Maoni

0 Maoni