TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.09.2022

mtzonline255.com
Lionel Messi

Mshambulizi wa Argentina Lionel Messi, 35, anatazamiwa kuondoka Paris St-Germain msimu wa ujao kwani atakataa ofa yoyote ya kandarasi mpya. (Beteve, via Star)

Mshambulizi wa Uingereza Harry Kane, 29, anasalia kuwa mlengwa namba moja wa Bayern Munich, huku miamba hao wa Ujerumani wakitarajiwa kujadiliana tena uamuzi wa Tottenham. (Kicker, via Sun)

Newcastle United wako tayari kutuma ofa ya tatu kwa kiungo wa kati wa Leicester City na Muingereza James Maddison, 25, baada ya ofa za £40m na ​​£45m kukataliwa. (Times - subscription required)

Jude Bellingham

Kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, anafaa kujiunga na Manchester United atakapoondoka Borussia Dortmund, kulingana na mlinda mlango wa zamani wa Old Trafford Ben Foster. (Metro)

Liverpool, ambao pia wamehusishwa na Bellingham, wameanza kulenga viungo wa kati mbadala na wanamfuatilia mchezaji wa Benfica wa Argentina Enzo Fernandez, 21. (Fichajes, via Teamtalk)

Chelsea haitapunguza bei wanayohitaji ya pauni milioni 31 kwa winga wa Marekani Christian Pulisic huku Juventus wakionyesha nia ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24. (Calciomercato, via Express)

mtzonline255.com
Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo

Klabu ya Saudi Arabia Al Hilal imedai mshambuliaji wa Manchester United Mreno Cristiano Ronaldo, 37, alikuwa na nia ya kujiunga nao msimu huu. (Mirror)

Mchezaji wa Eintracht Frankfurt Mdenmark Jesper Lindstrom, 22, amejibu ripoti zinazomhusisha na kuhamia Arsenal, akisema ni ‘’vilabu vikubwa kama wao vinanitazama’’. (Tipsbladet via Express)

Leeds wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya mkataba na winga wa Uingereza Jack Harrison, ambaye aliripotiwa kuwasilisha ombi la pauni milioni 20 kutoka Newcastle. Mkataba wa sasa wa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25 utakamilika msimu wa 2024. (Football Insider)

Mauricio Pochettino

Kocha mkuu wa zamani wa Tottenham na Paris St-Germain Mauricio Pochettino, ambaye amekuwa akihusishwa na kazi ya meneja wa England, alikuwa Wembley kutazama mechi yao na Ujerumani waliotoka sare ya 3-3. (Telegraph - subscription required)

Chelsea imemfuta kazi Thierry Laurent, akiwa wa nne wa timu hiyo kuondoka Stamford Bridge katika wiki moja iliyopita. (Mail)

Newcastle wanamfuatilia kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 18, anayechezea Vasco da Gama. (Fabrizio Romano)

Chapisha Maoni

0 Maoni