TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 29.09.2022

Mchezaji wa PSG Lionel Messi

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Lionel Messi, 35, huenda akarejea Barcelona kulingana na makamu wa rais Eduard Romenu, ambaye aliambia kituo cha redio cha Uhispania El Mati de Catalunya kwamba uhamisho wa mshambuliaji huyo wa Argentina "unawezekana." (The Sun) 

 Chelsea wamejiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili liungo wa England na Borussia Dortmund Jude Bellingham – bei ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 19- inakadiriwa kuwa pauni milioni  130, huku Liverpool na Real Madrid pia wakimtaka. (Telegraph - usajili unahitajika)

  Manchester City wanapanga kufanya mazungumza na kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva kubaini ikiwa atajaribu kuondoka klabu hiyo mwisho wa msimu huu, baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28-kuonyesha hamu ya kuondo kwa misimu miwili iliyopita. (Mail)  

Mchezaji wa Man City Benardo Silva

Barcelona wanavutiwa na kiungo wa kati wa Manchester City na Ujerumani Ilkay Gundogan, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akiwa amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake. (Sport) 


Wolves wameripotiwa kumsajili kiungo wa Chile Dario Osario kutoka Universidad de Chile kwa ada ya £5.5m huku Real Madrid na Manchester City hapo awali zikihusishwa na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18. (Express)

 Arsenal bado wanataka kumsajili Douglas Luiz,24, kutoka Aston Villa kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ghana anayeuguza jeraha Thomas Partey, 29. Koch awa Gunners Mikel Arteta alishindwa kumpata Luiz msimu uliopita lakini yuko tayari kuwasilisha dau la tatu la kumnunua kiungo huyo wa Brazil, baada ya ofa mbili kukataliwa siku ya mwisho ya uhamisho. (The Sun)
Mchezaji wa Aston Villa Douglas Luiz

Tottenham wanamnyatia mlinda mlango wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak, 29, kama mbadala wa muda mrefu wa kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, 35. (Evening Standard).

Rais wa Paris St-Germain Nasser al-Khelaifi amesema mauzo ya mali ya Barcelona msimu wa joto ili kufadhili usajili wa wachezaji "sio sawa" na kupendekeza Uefa ichunguze uhalali wao. (ESPN)  
Mlinda mlango wa Atletico Madrid Jan Oblak

Tottenham wanatazamia kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Dejan Kulusevski, 22, kwa mkataba wa kudumu wakati mkopo wake kutoka Juventus utakapoisha. (Fabrizio Romano

Atletico Madrid wanafikiria kumnunua mlinda mlango wa Manchester United David de Gea huku kandarasi ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 31 ikikamilika mwishoni mwa msimu huu. ( 90 Minutes)  

Chelsea wanaweza kumsajili tena mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 24, kutoka Roma kupitia kifungu cha kumnunua tena kwa pauni milioni 67. (Fabrizio Romano)  

Chapisha Maoni

0 Maoni