Mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji Romelu Lukaku hana mpango wa kurejea Chelsea atakapokamilisha mkopo wake wa msimu mzima Inter Milan. Klabu hiyo ya Italia inatarajiwa kuongeza muda wa mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (La Gazzetta dello Sport, via Football Italia)
Mshambulizi wa Brighton na Ubelgiji Leandro Trossard, 27, anasema yuko tayari kumfuata kocha wa zamani wa Seagulls Graham Potter hadi Chelsea, lakini angetaka kucheza na si kukaa kwenye benchi. (Het Nieuwsblad, via Mail)
Manchester City wamefikia makubaliano kimsingi juu ya mkataba mpya wa mshambuliaji wa England Phil Foden, na mkataba huo unaaminika kuwa wa zaidi ya miaka sita na thamani yake ni pauni 250,000 kwa wiki. (Football Insider)
Beki wa Liverpool Vigil van Dijk, 31, mlinzi mwenzake Mholanzi Jurrien Timber, ambaye alihusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United msimu wa jot , anaimarika zaidi katika ukuaji wake kuliko alivyokuwa akiwa na umri uleule wa miaka 21. (Manchester Evening News)
Beki wa Argentina Lisandro Martinez, 24, anasema hakuzingatia kukosolewa kwake mwanzoni mwa msimu baada ya kuhamia Manchester United msimu wa joto kutoka Ajax. (TyC Sports, via Metro)
Leicester City inaweza kuchukua hatua kujaribu kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani Robin Gosens, 28, ambaye anaweza kucheza katika safu ya ulinzi au kiungo wa kushoto, kutoka Inter Milan mnamo Januari. (FC Inter News)
Kiungo wa kati wa Serbia Nemanja Matic, ambaye alijiunga na Roma majira ya joto baada ya kandarasi yake ya Manchester United kuisha, yuko mbioni kuanzisha upya kandarasi moja kwa moja katika klabu hiyo ya Serie A. (La Gazzetta dello Sport, kupitia Football Italia)
Rangers wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Finland mwenye umri wa miaka 26 Glen Kamara katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Insider)
0 Maoni