Shirikiso la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeandika barua kwa klabu ya Yanga ikiwazuia kumleta winga wao nchini Tanzania Tuisila Kisinda kwa madai kuwa hawawezi kumtumia kwenye ligi kuu inayotarajiwa kurejea septemba 6 mwaka huu.
Gazeti la mwanaspoti limeripoti kuwa TFF imezuia klabu hiyo kwa madai kuwa tayari yanga ilishakuwa na wachezaji wengine waliiombewa uhamisho licha ya Yanga kudai kuwa ilishamwondoa mshambuliaji wao Lazarous Kambole kutoka Zambia ili kumsajili kisinda.
"Wakati tunamsajili Kisinda tulishapanga tumuondoe nani,na huku kwetu tulishamwondoa Kambole kwakua tuliona hali yake ya majeruhi itatupa shida,tumemwondoa kwenye mfumo ili nafasi yake aichukue kisinda" imesema klabu ya Yanga
Taarifa zinasema kuwa Klabu hiyo imepanga kutoa malalamiko katika kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji kupinga uamuzi huo.
Chanzo : Mwanaspoti
0 Maoni