Liz Truss ameteuliwa rasmi kuwa waziri mkuu mpya wa Uingereza,baada ya kukutana na malkia Elizabeth wa pili aliemuumba kuunda serikali mpya wakati taifa hilo likipambana na mfumuko wa bei.
Truss mwenye umri wa miaka 47 amechukua madaraka siku moja baada ya chama chake cha Conservative kumpitisha kama kiongozi wake.
Mtangulizi wake Boris Johnson ajiuzulu rasmi baada ya kwenda Scotland kukutana na malkia na kumkabidhi rasmi barua yake ya kujiuzulu.
Akizunguza nje ya ofisi yake ya mtaa wa Downing kabla ya kuelekea Scotland, Johnson alisema amefanya mengi katika muda wa miaka mitatu madarakani yalioicha Uingereza na nguvu ya kiuchumi itakayo wasaidia watu kupambana na mzozo wa nishati.
0 Maoni