TANGAZA HAPA

Vodacom ya kwanza kuzindua 5G

 


Kampuni ya Vodacom Tanzania imefanya uzinduzi rasmi wa biashara wa teknolojia ya 5G na kuifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi chache Afrika zinatumia huduma hii ya mtandao yenye kasi zaidi duniani.

Uzinduzi huo wa kihistoria umefanyika leo Septemba 1,2022 katika ukumbi wa Mlimani City jini Dar Es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari mweshimiwa Nape Moses Nnauye.

Katika namna ya kuvutia sana iliyoibua shangwe ukumbini hapo ilitangazwa kwamba kutokana na majukumu ya kitaifa mweshimiwa Nape Nnauye ameshindwa kufika kwa wakati hivyo akalazimika kutoa hutoba yake ya awali mbali na ukumbi huo lakini teknolojia ya 5G ilimfanya aonekane ukumbini hapo kwa mfumo wa "Hologram" ikiwa ni mara ya kwanza kabisa kufanyika Tanzania.

Katika hotuba aliyotoa kabla ya kufika ukumbini waziri Nape Nnauye alisema ilikuwa ngumu kufikiria kama dunia ingefikia katika hatua hii huku akiipongeza Vodacom kwa kuleta mapinduzi haya Tanzania."Nakumbuka mwezi wa tano mwaka huu (2022) tuliahidi mwaka huu wa fedha Tanzania itaanzisha huduma ya 5G.wakati ule tulipokuwa tukisema ilikuwa kama ndoto 'now it is only tree months' (sasa ni miezi mitatu tu)toka tuliposema Vodacom wametenda wametusaidia kuingia kwenye orodha ya nchi chche zaidi Afrika ambazo zimeanzasha teknolojia ya 5G" Alisema Nape Nnauye.

Baadae waziri Nape Nnauye alifika ukumbini hapo na kumalizia hotuba yake, "Serikali kupitia wizara inaunga mkono kikamilifu sekta binafsi na mfumo wa kiteknolojia ya uvumbuzi kwasababu tunajua teknolojia kama vile mtandao wa vit (IoT),akili bandia (Artifical Intelligence) na kujifunza kwa mashine (Mashine Learning),Ekolojia ya Blockchain,mtandao wa 5G ,roboti na kompyuta zinazoongezwa katika kutoa masuluhisho na kusaidia nchi kufikia katika malengo yake SDG kwahiyo leo tunaunga mkono kikamilifu maendeleo haya na tunapozingua rasmi kibiashara (market launch) teknolojia hii ya 5G hapa nchini na upatikanaji wa mtandao wa kasi ukijulikana kama "Wireless ya Fibre" hii inadhihirisha kuwa kampuni ya Vodacom Tanzania inazidi kuongoza katika katika huduma ya teknolojia hapa nchini."

Mkurugenzi wa mtandao wa Vodacom Tanzania Naye Andrew Lupembe alieleza kwamba Vodacom inajivunia kuwa ya kwanza kutambulisha rasmi kibiashara mtandao wa 5G na kuweka wazi kwamba watawekeza zaidi ya vituo 200 vya 5G ndani ya Tanzania hadi kufikia mwezi Novemba 2022.

Kutokana na mapinduzi hayo makubwa Tanzania sasa inaungana na nchi za Botswana,Eygt,Ethiopia,Gabon,Kenya,Lesotho,Madagasca,Mauritius,Nigeria,Senegal,Seychelles,Afrika kusini,Uganda na Zimbabwe kuwa nchi chache afrika kuwa na matandao wa 5G.

Chapisha Maoni

1 Maoni