Washtakiwa wanne kati ya watano katika kesi ya uhujumu uchumi ilikuwa ikimkabili aliekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya wametiwa hatiani baada ya kukiri kutenda makosa mawili.
Washtakiwa hao wamekubali kulipa faini ya Sh 50,000 pamoja na kumlipa mhanga Alex Swai kiasi cha Sh milioni moja (1) kwa kila mmoja.
Washtakiwa hao Sylvester Nyengu, John Aweyo, Nathan Msuva na Antero Assey ambapo wamekuwa na makosa mawili jumanne Septemba 6,2022 katika mahakama ya hakimu mkazi moshi mkoa wa Kilimanjaro.
Hata hivyo washtakiwa hao mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo salome mshasha wamekubali kulipa Sh 1,050,000 kwa kila mmoja.
0 Maoni