TANGAZA HAPA

Yanga yaanza kwa kishindo ligi ya Mabingwa Afrika


 Mabingwa wa Tanzania bara Yanga SC wameanza vyema katika kuwania kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuwachapa wenyeji wao Zalan Fc 4-0 kutoka nchini Sudan kusini mchezo wa mkondo wa kwanza.

Yanga walipata mabao yote katika kipindi cha pili huku mshambuliaji wao Fiston Mayele akifunga Hat-trick dakika 46,85 na 88 huku bao jingine likifunga na Feisal Salum dakika ya 55.

Yanga watarudiana na Zalan Fc Septemba 16, 2022 katika uwanja wa Benjamin mkapa jijini Dar Es Salaam.

Chapisha Maoni

0 Maoni