TANGAZA HAPA

Amchoma mtoto wake moto kwa kuiba sh.250 na kudokoa mboga

Mtoto aliechomwa moto mikono na mama yake

 Mkazi mmoja wa Kijijii cha Namanjele mkoani Mtwara, Somoe Mohamed amemchoma mikono mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano kwa madai ya kudokoa mboga na kuiba kiasi cha shilingi 250.

Akiongea na chombo kimoja cha habari leo (jana) Oktoba 4, 2022 Somoe amekiri kufanya ukatili huo, akisema lengo lake lilikuwa ni kumwadhibu mtoto kwa tabia mbaya aliyoionyesha.

“Nilikuwa namwadhibu kwa tabia yake. Siku ya kwanza alichukua Shilingi 50 na siku ya pili alichukua Shilingi 200 na baadae akaanza kudokoa dagaa nikamuonya, lakini hakusikia mpaka sasa mtoto anasiku tatu tangia amechomwa moto,” amesema mama Somoe.

Kwa upande wake Baba wa mtoto huyo, Juma Lubega, amesema kuwa yeye alisikia kuwa mwanaye amechomwa moto na mama yake lakini hakuamini hadi alipofika nyumbani alimuona mtoto akiwa ameungua sehemu ya mikono yake vikiwemo vidole.

“Nilisikia uchungu kama baba nilipouliza nikaambiwa kuwa kaiba Shilingi 250 na kudokoa dagaa, yaani inaonyesha kuwa alimfunga kamba mikononi akaweka nyasi akamchoma mtoto na inaonyesha alipowasha moto aliondoka ndio maana mtoto amepata madhara makubwa,” amesema Lubega.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Mkadimba amesema kuwa tukio hilo sio zuri kwakuwa halifundishi mtoto bali linaweza kumfanya akawa katili.

“Huyu mtoto tangia achomwe hajapelekwa hosptiali yoyote wala hajapata dawa zaidi ya miti shamba wanayotumia kumuwekea mikononi kutokana na imani kuwa atapona kwa kutumia dawa za asili,” amesema.


CHANZO: Nipashe

Chapisha Maoni

0 Maoni