TANGAZA HAPA

Burkina Faso: Aliepindua nchi akutana na baraza la mawaziri

Kapteni wa jeshi Burkina Faso Ibrahim Traore

Mkuu wa serikali ya Burkina Faso na aliyejitangaza kuwa kiongozi mpya, Ibrahim Traore, alikutana na maafisa wa baraza la mawaziri siku ya Jumapili kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Aliyekuwa kiongozi wa junta Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba pia alijitolea kujiuzulu kufuatia mazungumzo na kiongozi huyo mpya.

 Ibrahim Traore alisema “Kwa kweli tunatakiwa kubadili mwendo, tunatakiwa kubadili mwendo, tunatakiwa kwenda haraka, nchi nzima iko katika hali ya hatari, hivyo kila mtu katika ngazi hii lazima awe na kasi na kuachana na mkanda mwekundu usio wa lazima.

"Siwezi hata kutaja nukta moja, sehemu moja ambapo ni muhimu kuwa haraka Hapa Burkina, kila kitu ni cha haraka. Kuanzia usalama hadi ulinzi, afya, hatua za kijamii, miundombinu, kila kitu ni cha dharura"

Saa chache kabla ya matukio kutokea Ijumaa iliyopita, mamia ya watu walikusanyika katika mji mkuu, Ouagadougou, wakitaka Damiba aondoke, na mwisho wa uwepo wa kijeshi wa Ufaransa katika Sahel huku wakiomba  ushirikiano wa kijeshi na Urusi.

Hii ni mara ya pili katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja ambapo Burkina Faso imekuwa na mabadiliko ya uongozi.

Zaidi ya 40% ya Burkina Faso bado iko nje ya udhibiti wa serikali.

Chapisha Maoni

0 Maoni