TANGAZA HAPA

DODOMA: Wawili mbaroni kwa tuhuma za mauaji

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), Martin Otieno

Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, linawashikiliwa watu wawili kwa tuhuma za mauaji wa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16).

Mwanafunzi huyo aliuawa usiku wa juzi Jumanne, Oktoba 4, 2022 nyumbani kwao Mtumba jijini Dodoma na watu wasiojulika,Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akifanya biashara zake katika klabu cha pombe.

Mjomba wa Farida, Anderson Makuya alisema usiku wa kuamkia juzi alipokea simu kutoka kwa ndugu zake wakimjulisha kuwa mpwaye amepigwa na watu wasiojulika na amepelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, lakini alipoteza maisha wakiwa njiani.


CHANZO: Mwananchi

Chapisha Maoni

0 Maoni