TANGAZA HAPA

GEITA: Mama amchoma moto mikono mwanae kisa Sh 30,000

Helena Mashaka aliechomwa moto mikono na mama yake

Helena Mashaka (13), mwanafunzi wa darasa la saba shule ya Shahende iliyopo Kata ya Butobela, mkoani Geita, amechomwa mikono yake kwa moto na Mama yake kwa tuhuma za kuiba shilingi 30,000 na kupelekea mwanafunzi huyo kushindwa kufanya mitihani yake ya kuhitimu.

Mtendaji wa Kijiji hicho Edgar Michael, amesema alipata taarifa ya mtoto huyo kujeruhiwa kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo majira ya saa 2:00 asubuhi akidai kuwa kuna binti amechomwa moto na Mama yake na ameshindwa kufanya mitihani.
Baada ya kupata  taarifa hiyo wakamfuatilia mzazi kisha wakamkamata na baada ya mahojiano mama huyo alidai kuwa alifanya tukio hilo kwa sababu mtoto huyo aliiba shilingi 30,000.

Mpaka sasa mzazi huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kata ya Bukoli, na mwanafunzi amepelekwa Zahanati ya Bukoli kwa ajili ya kupatiwa matibabu 

Chapisha Maoni

0 Maoni