TANGAZA HAPA

Mapendekezo ya Serikali juu ya vifurushi vya Bima ya afya kwa wote


Prof. Makubi amesema uchangiaji unaopendekezwa ni Sh. 340,000 kwa kaya ya watu 6 ikiwemo mchangiaji mwenza wake na wategemezi wasizidi wanne kwa mwaka pindi sheria hiyo itakapojadiliwa na kupitishwa na Bunge 

Vilevile kwa mtu mmoja asiye na familia atachangia  Sh 84,000 kwa mwaka.Kiwango hiki ukilinganisha na gharama za matibabu ni ndogo na serikali bado itafidia gharama nyingine.

Prof. Makubi amebainisha kuwa kwa wananchi watakaotambuliwa kutokuwa na uwezo wataendelea kupatiwa huduma kwa utaratibu utakaowekwa na Serikali kwa kila mtu kuwa na kadi yake ya Bima ya Afya.

"TASAF na mifumo ya maendeleo ya jamii ndio itakayofanya utambuzi kwa wananchi wasio na uwezo ili kuiwezesha Serikali kuweka utaratibu madhubuti wa kutoa huduma kwa wananchi wasio na uwezo kupata huduma pindi wanapohitaji". Prof. Makubi.

"Sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote inaenda kuwakomboa wananchi, inaenda kuhakikisha kila mwananchi, Mtanzania anakuwa na Bima ya afya, kwa sasa hivi takribani 15% tu ya wananchi wanabima za afya mbalimbali, inawaacha 85% ya Watanzania kutokuwa na uhakika wa kutibiwa pale.



Chapisha Maoni

0 Maoni