TANGAZA HAPA

Mwanajeshi ahukumiwa kunyongwa hadi kufa


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi cha 08/691 KJ Chandarua Mkoani Ruvuma, Sajenti Batsin Sanga amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwaua kwa risasi Mtalaka wake na Mwanajeshi mwenzake.

Ingawa jina la Askari aliyeuawa pamoja na Veronica halitajwi kwenye hukumu, ushahidi unaonesha Askari huyo alifyatua risasi 10 kati ya 30 alizokabidhiwa huku miili ya marehemu ikikutwa na majeraha ya risasi kichwani, hukumu imetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea, Yose Mlyambina aliyesema adhabu kwa anayepatikana na hatia ya mauaji ya kukusudia ni moja tu, nayo ni kunyongwa hadi kufa.

Akitoa hukumu hiyo Jaji Yose amesema “Mapenzi ni hisia kali sana za ndani ambazo hazielezeki, kwa lugha rahisi mapenzi ni kitu kizuri sana na chenye harufu nzuri ya kuvutia na ambacho kinadumu milele bila kujali mazingira, ingawa siku hizi Jamii imethibitisha kinyume chake, mapenzi yamekuwa bidhaa inayoharibika, inaoza na kuzama, utamu umekuwa uchungu kiasi cha kusababisha Wapendanao kuuana wao kwa wao”

Siku mauaji hayo yanatokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Mshitakiwa atalakiane na Veronica, jana yake Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea ilitoa haki ya Mke kutunza Mtoto, Veronica akiwa na Rafiki yake aitwaye Jamila Said walienda kwenye kambi hiyo alipokuwa akifanya kazi Mshitakiwa ili kupeleka amri hiyo na alimuona Mtalaka wake ghafla Mshtakiwa alichukua bunduki na kumfyatulia risasi Veronica kisha akamfyatulia risasi Askari mwenzie na wote wawili kufariki huku Jamila akifanikiwa na kukimbia.

Chapisha Maoni

0 Maoni