Polisi katika mji mkuu wa Kenya wanasema wanamtafuta mtunza fedha wa kanisa anayeshukiwa kuiba Ksh 1.5m ($12,400; £11,240) ambazo waumini walikuwa wamechangisha ili kuendeleza kanisa.
Polisi wanamshtumu mwanamume huyo kwa kuvunja kanisa la ACK All Saints Mountain View huko Kangemi, viungani mwa jiji la Nairobi, na kuchukua pesa kutoka kwa droo kwenye madhabahu.
Mzee wa kanisa na mweka hazina "walishtushwa" walipoingia Jumatatu asubuhi kuchukua pesa, na kukuta kanisa likiwa limeibiwa na pesa hazipo, polisi walisema.
Katika taarifa yake, Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ilisema uchunguzi wao wa awali ulielekeza mlinzi wa kanisa hilo kuwa mshukiwa mkuu. "Anashukiwa kuvuruga nguvu za umeme za kanisa kuzima mfumo wa CCTV uliowekwa kabla ya kuondoka na michango ya waumini," walisema.
CHURCH CARETAKER TAKES OFF WITH CASH RAISED YESTERDAY BY CONGREGANTS
— DCI KENYA (@DCI_Kenya) October 10, 2022
Detectives based at Kangemi police station in Dagoretti sub county, have launched a manhunt for a suspect who broke into a church and made away with over Sh1.5 million.
Source:bbcswahili
0 Maoni