Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amesema atamalizana na mchezaji wake Cristiano Ronaldo baada ya kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu katika pambano dhidi ya Totenham Hotspurs lililomalizika kwa Manchester United kushinda kwa mabao 2-0.
Katika mchezo huo Ronaldo alionekana kuondoka uwanjani na Kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa ni dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhishwa na kukaa benchi.
Akijibu swali kwa mwandishi wa Habari wa Amazon Prime, Ten Hag alinukuliwa akisema:
“Alikuwepo pale, nilimuona lakini sikuongea naye.”
Huwa sitilii maanani vitu kama hivyo, nitalifanyia kazi hilo suala kesho (leo), nataka kila kitu kielekezwe kwenye timu.
Ronaldo amekuwa na tabia ya kutawala vichwa vya Habari vya mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya Habari kutokana na kuwa na baadhi ya matukio ambayo yanaonesha utovu wa nidhamu hasa nje ya uwanja kutokana na ukubwa wa jina lake.
Hatua hiyo inajiri siku tatu baada ya kuonyesha kutofurahishwa na kutolewa katika mechi dhidi ya Newcastle. Baada ya sare ya 0-0 Jumapili Ten Hag alisema hana tatizo na majibu hasi ya Ronaldo, lakini akaongeza Mreno huyo lazima amshawishi lazima asalie. Mshambulizi wa zamani wa England, Gary Lineker alisema tabia ya Ronaldo hakupaswa kuonekana wakati ambapo timu yake ilikuwa inacheza dhidi ya Spurs.
“Samahani, hiyo haikubaliki – ni tabia mbaya sana,” Lineker alisema kwenye Mechi ya Siku ya Jumatano. Wachambuzi Ashley Williams na Micah Richards walikubaliana na Lineker.
“Kwa mmoja wa magwiji wa mchezo kufanya hivyo wakati timu yake inashinda, inakatisha tamaa,” alisema beki wa zamani wa Uingereza Richards. Nahodha wa zamani wa Wales Williams aliongeza: “Ulikuwa usiku mzuri sana kwa Manchester United na hapa tunazungumza tena kuhusu Cristiano Ronaldo – ingawa hakucheza.”
0 Maoni