TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 08.10.2022

Mshambuliaji wa Manchester United Cristiano Ronaldo

Manchester United wana imani Cristiano Ronaldo, 37, atasalia katika klabu hiyo mwezi Januari kwa sababu ya kutovutiwa kwa klabu zingine na fowadi huyo wa Ureno. (ESPN)

Paris St-Germain wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, msimu ujao. (Foot Mercato - in French)

Newcastle United wamefanya mazungumzo na Vasco da Gama ya Brazil kuhusu uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 18, ambaye anatarajiwa kugharimu £30m.

Forward wa Chelsea Pierre-Emerick Aubameyang

Meneja wa Leicester City Brendan Rodgers anasema anakubali kwamba kiwango kizuri cha kiungo wa kati wa Uingereza James Maddison kitavutia maombi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 mwezi Januari. (Mail)

Chelsea wanatazamiwa kumteua Christopher Vivell kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo baada ya Mjerumani huyo kutimuliwa na RB Leipzig. (Telegraph - subscription required)

Winga wa Napoli na Mexico Hirving Lozano, 27, anaweza kuishia Manchester United au Everton msimu ujao, wakala wake wa zamani amependekeza.. (Mirror)

Xabi Alonso

Rafael Benitez na meneja mpya wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso walikuwa miongoni mwa majina yanayofikiriwa kuchukua nafasi ya Steve Cooper huko Nottingham Forest kabla ya klabu hiyo kuamua kumpa mkataba mpya. (Mail)

Tottenham watalipa Juventus £30.7m kumnunua winga wa Uswidi Dejan Kulusevski, 22, kwa mkataba wa kudumu. (Calciomercato - in Italian)

Makamu wa rais wa Barcelona Eduard Romeu ana imani klabu hiyo inaweza kutafuta njia ya kumrejesha mshambuliaji wa Paris St-Germain wa Argentina Lionel Messi, 35, ikiwa wanataka. (90min)

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi

Mwana wa David Beckham, Romeo, anafanya mazoezi na timu B ya Brentford baada ya kumalizika kwa msimu wa Major League Soccer Next Pro. (Guardian)

Leicester wanakamilisha dili la kumsajili golikipa wa Poland Bartlomiej DrÄ…gowski kutoka Spezia ya Italia mwezi Januari. (Meczyki - in Polish)

Atletico Madrid wametia saini mkataba wa pauni milioni 17.5 kubadilisha mkopo wa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann kutoka Barcelona kuwa uhamisho wa kudumu. (Marca - in Spanish)

Chapisha Maoni

0 Maoni