TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 03.10.2022

Anthony Martial

Sevilla na Valencia wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26, kutoka Manchester United (Todofichajes - in Spanish)

Kocha wa zamani wa Olympiacos Pedro Martins huenda akawa mshindani mkubwa kuchukua nafasi ya Bruno Lage kama meneja wa Wolves, huku kocha wa Sevilla Julen Lopetegui akizingatiwa na Ange Postecoglou wa Celtic akiwa katika mazungumzo. (Telegraph - subscription required)

Kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim pia ni miongoni mwa wanaowania kazi ya Wolves, ingawa itaigharimu klabu hiyo pauni milioni 20 kama fidia. (Sun)

Christopher Nkuku

Chelsea walitaka kuweka siri habari kuwa Christopher Nkunku tayari amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na klabu hiyo kwa kuwa bado hawajakubaliana ada na RB Leipzig kwa ajili ya fowadi huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. (Fabrizio Romano)

Liverpool itakabiliana na ushindani kutoka kwa Juventus na Real Madrid kuwania saini ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye kandarasi yake ya Leicester inamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Calciomercato - in Italian)

Klabu ya UAE Sharjah FC imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Everton Salomon Rondon, ingawa mchezaji huyo wa kimataifa wa Venezuela mwenye umri wa miaka 33 anaonekana huenda akasalia Goodison Park. (Liverpool Echo)

Balogun

Reims wanataka kubadilisha mkopo wao wa msimu mzima wa mshambuliaji wa Arsenal Folarin Balogun, 21, kuwa uhamisho wa kudumu. (Ekrem Konur)

Arsenal wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea, Bayern Munich na PSG kwa mshambuliaji wa Juventus Dusan Vlahovic, 22. (Il Bianconero - in Italian)

Manchester United ilishindwa katika jitihada za kumsajili kiungo wa kati wa Italia Manuel Locatelli, 24, kutoka Juventus msimu wa joto. (Sport Mediaset - in Italian)

Locatelli

Arsenal wameulizia kuhusu kumsajili Locatelli katika dirisha la usajili la Januari. (Calciomercato - in Italian)

 Winga wa Tottenham Mbrazil Lucas Moura, 30, atalengwa na Sevilla katika dirisha la uhamisho la Januari. (Vamos Mi Sevilla - in Spanish)

Chapisha Maoni

0 Maoni