Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewaonya wamiliki wa vyombo vya usafiri wanaotumia namba ambazo hazijatolewa na TRA ama Taasisi nyingine za Serikali, ambazo zimepewa jukumu hilo kisheria.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka hiyo, iliyochapishwa katika mitandao ya kijamii Oktoba 5, 2022 imesema imebaini uwepo wa magari barabarani, yaliyobandikwa namba kwa kutumia kwenye vibati ambavyo vina rangi tofauti nazinazotolewa kisheria.
TRA imesema, “Kumekuwepo na matumizi ya vibati vya namba vyenye rangi zisizotambulika kisheria vinavyowekwa mbele na nyuma ya vyombo vya moto, utengenezaji na matumizi ya vibati hivyo ni kosa kisheria kama inavyoelezwa kwenye Kifungu cha 8 cha Sheria ya Usalama Barabarani (The Road Traffic Act, 1973),”
TRA imesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayeendelea kukiuka sheria hiyo, ikiwa ni pamoja na kutaifisha chombo cha moto husika.
0 Maoni