TANGAZA HAPA

UTURUKI: mlipuko waua 28 ndani ya mgodi

Takriban watu 28 wamefariki na wengine makumi kadhaa bado wamekwama chini ya ardhi ndani ya mgodi baada ya mlipuko kutokea ndani ya mgodi huo wa makaa ya mawe uliopo katika jimbo la kaskazini mwa Uturuki la Bartin.

Karibu watu 10 walikuwa ndani ya mgodi wakati mlipuko huo ulipotokea Ijumaa, na karibu nusu yao walikuwa zaidi ya mita 300 chini.

Waziri wa afya wa Uturuki Fahrettin Koca alisema kuwa watu 11 wameokolewa na wanaendelea kupatiwa matibabu.

Watoa msaada wakiwa eneo la tukio kusaidia waliokwama mgodini

Wahudumu wa uokozi waliendela na kazi ya kuwaokoa watu usiku kucha, wakichimba kwenye miamba kujaribu kuwafikia manusura zaidi.

Picha za video zinaonyesha wachimba migodi wakiokolewa huku baadhi wakiwa wameungua na wengine walionekana wenye uchovu huku wakisindikizwa na waokoaji kwenye eneo la uokozi lililopo kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi.

Famili na marafiki wa wachimba migodi ambao hawajulikani walipo pia wanaonekana kwenye mgodi, wakisubiri kwa shauku kusikia taarifa za wapendwa wao.


Chapisha Maoni

0 Maoni