TANGAZA HAPA

Wawili kizimbani kwa tuhuma za ubakaji


Wanaume wawili wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma,  wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kulawiti mwanafunzi wa darasa la nne na wa kidato cha pili.

Washtakiwa hao Mathias Mkokoteni (43), mkazi wa Kata ya Mpwapwa Mjini, Mtaa wa  Igovu, anadaiwa  kubaka  na kulawiti mtoto wa miaka 13, anayesoma shule ya msingi Igovu kati ya  mwezi Juni na Julai, huku mshtakiwa Christian Mgongo (18), anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Berege mwenye umri wa miaka  14.
Kesi hizo zinasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mpwapwa, Nurupudesia Nasaary.

Akimsomea shitaka lake, mwendesha mashitaka wa polisi Joseph Michael, alidai mahakamani kuwa, Mkokoteni,  alifanya tukio hilo katika Mtaa wa Igovu, Kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa, ambapo alimbaka na kumlawiti binti mwenye umri wa miaka 13.

Kwa upande wake Mgongo, ilidaiwa alifanya tukio hilo katika Kijiji cha Berege, Wilaya ya Mpwapwa, Septemba 24, mwaka huu kwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Mazae.

Chapisha Maoni

0 Maoni