TANGAZA HAPA

Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss ajiuzulu

Aliekuwa Waziri mkuu wa Uingereza Liz Truss
Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss amejiuzuu wadhifa wake kama kiongozi mkuu wa Chama cha Conservative na Waziri Mkuu wa nchi hiyo leo Oktoba 20, 2022 zikiwa ni siku 44 tu tangu alipochaguliwa kushika wadhifa huo.

Hatua hiyo imekuaja baada ya kumfukuza kazi Kwasi Kwarteng, Kansela wa Hazina ya Uingereza ambaye alifutwa kazi na Truss Oktoba 14, 2022 baada ya kutangazwa kwa bajeti ndogo ya serikali ambayo iliahidi kupunguza kiasi kikubwa cha kodi kwa matajiri.
mtz online 255

Bajeti hiyo ilisababisha upinzani mkubwa kutoka kwa umma na soko katika wiki za hivi karibuni.
Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss akitoka nje ya kasri kutangaza kujiuzulu kwake katika huko Downing Street hii leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 jijini London
Kujiuzulu kwa waziri mkuu huyo, kunamfanya Truss kuwa waziri mkuu aliyekaa madarakanai kwa muda mfupi zaidi nchini Uingereza ambapo alichukua madaraka Septemba 5, 2022 akichukua nafasi hiyo kutoka kwa Boris Johson ambaye naye alilazimishwa kujiuzulu.

Katika hotuba yake ya kujiuzulu, Truss ameeleza kuwa atahakikisha waziri mkuu mpya wa Uingereza anapatikana ndani ya wiki moja kutoka sasa.

Wanasiasa wanaopewa nafasi kubwa ya kurithi kitu hicho, ni pamoja na kansela Rishi Sunak anayepewa nafasi kubwa zaidi ambaye alichuana vikali na Truss katika uchaguzi wa kiongozi mkuu wa chama cha Conservative, akifuatiwa na Penny Mordaunt na Ben Wallace.



Chapisha Maoni

0 Maoni