TANGAZA HAPA

Ahukumiwa kifungo cha maisha mara mbili kwa kulawiti mwanafunzi

Emanuel Gwandu (21) amehukumiwa kifungo cha maisha mara mbili pamoja na kulipa fidia ya TZS milioni 5 baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.

Gwandu mkazi wa Mtwivila mkoani Iringa alikuwa akisimamia sehemu ya kuchezesha michezo ya video alidaiwa kumrubuni mwanafunzi huyo na kumpa nafasi ya kucheza bila malipo na kisha kumpeleka vichakani na kumuingilia kinyume na maumbile.

Mahakama imemshutumu mtuhumiwa na makosa mawili aliyotenda kwa tarehe tofauti mwezi agosti na kosa la pili septemba 27 ambapo alimuingilia mwanafunzi huyo mara 6 kinyume cha maumbile.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi mkuu Said Mkasiwa amesema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mtuhumiwa alitumia fursa ya mwanafunzi huyo ya kukosa pesa na mapenzi yake ya kucheza Playstation kumfanyia tukio  hilo.

Aidhaa mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia adhabu kwakuwa hajatenda kosa lolote.


Chapisha Maoni

0 Maoni