Juma Ligamba (40) mkazi wa kijiji cha Kibubwa wilayani Butiama amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Musoma mkoani mara baada ya kukutwa na hatia ya kosa la kumbaka mlemavu wa viungo na akili.
Mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Denis Bigando amesema kuwa mshtakiwa huyo alimbaka msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 Septemba 20, 2022 majira ya jioni katika kijiji cha Kibubwa wilayani humo.
Akielezea tukio hilo amesema siku ya tukio mshtakiwa ambaye ni jirani wa mhanga alifika katika nyumba hiyo baada ya kubaini kuwa mama wa binti huyo hakuwepo na hivyo kuingia ndani moja kwa moja alipokuwa amelala binti huyo kisha kumbaka.
Hukumu hiyo ilitolewa jana Novemba 9, 2022 na hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo Stanley Mwakihaba ambapo alisema mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo na hivyo anastahili kutumikia kifungo hicho kwa mujibu wa sheria.
0 Maoni