Mbunga wa viti maalum Judith Kapinga amesema mkandarasi mkuu aliyepewa tenda ya kufanya maboresho katika bandari ya Tanga kwa kish cha TZS Bilioni 104 alizopewa kutoka serikalini aliigawa kazi hiyo kwa mkandarasi mwingine kwa kiasi cha TZS Bilioni 40 pekee.
Akifafanua hayo leo Bungeni Dodoma wakati wa kujadili taarifa za kamati zilizotokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mwaka 2020/21 amesema kuwa kampuni hiyo iliyotambulika kwa jina la CHEC iliingia mkataba wa mwaka mmoja na mamlaka ya Bandari Tanzania Agosti 3, 2019 hadi Agosti 3, 2020 kwaajili ya kazi kuu tatu ambazo ni kuongeza kina che lango na sehemu ya kugeuzia meli ,kufanya tathmini ya athari ya kimazingira na kununua vifaa kwaajili ya shughuli za bandari.
Ameongeza kuwa kazi iliyotakiwa kufanyika ilikuwa na thamani ya TZS Bilioni 176.36 huku kazi aliyompa mkandarasi mbia ilikuwa ni kuongeza kina na ujenzi wa gati ambayo iligharimu asilimia 60 ya fedha zote licha ya kuwa mkandarasi huyo kutakiwa kupokea TZS Bilioni 104 badala yake alipewa fedha pungufu ambazo ni TZS Bilioni 40 huku mkandarasi mkuu CHEC Akitokomea na kiasi cha TZS Bilioni 64.
Aidhaa kapinga amehoji kwanini jambo hilo halikuwekwa kwenye ripoti ya kamati wakati wa majumuhisho yao ikiwa ni jambo ambalo linaguasa maslahi ya watanzania na fedha za Umma huku akidai viongozi wa mamlaka husika kuukalia kimya ubadhilifu huo.
Mbunge huyo ameliomba Bunge kuazimia hatua za haraka zichukuliwe kwa wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.
0 Maoni