Picha Ya ndege ya Precision Air iliyopata ajali ziwa Victoria
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema tayari miili 19 ya waliofariki katika ajali ya ndege ya kampuni la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria mapema Asubuhi ya leo Novemba 06, 2022, imepatikana huku akiagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini watu wawili wanaozidi kwenye idadi iliyoainishwa mwanzo kuwa ndege ilikuwa na watu 43, ikiwa ni tofauti na idadi ya sasa ambayo ikijumlishwa, waliookolewa 26 na waliofariki 19 ni watu 45.
0 Maoni