Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefika mkoani Kagera katika eneo ajali ya ndege ilipotokea na kuahidi kuwa baada ya uchuguzi watatoa taarifa ya chanzo cha ajali hiyo. Aliongeza pia wanafatilia imekuaje hadi idadi ya watu waliokua kwenye orodha rasmi kuongezeka kutoka 43 hadi 45.
Taarifa rasmi kutoka kwa mamlaka na shirika la ndege la Precision ilionesha kuwa abiria ni 43, lakini baadae ilitajwa idadi ya 45 jumla.
Kwa mujibu wa Waziri mkuu Majaliwa na Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamilawatu 19 wamefariki, na 26 waliokolewa.
‘’Tunashukur Mungu kwa kutuokolea abiria 26, Orodha ya mwanzo ilionesha abiria 43 lakini baada ya kuwakoa 26, kule ndani tulitarajia 17 lakini tukatoa miili 19, hawa wawili wametoka wapi? bado tunachunguza hawa wawili na tutatoa taarifa zaidi’’ anasema Waziri Majaliwa.
Hata hivyo zoezi la uokoaji linaendelea na kwa mujibu wa mamlaka nchini Tanzania, sasa mizigo na vifaa vingine vinaendelea kuopolewa ndani ya maji.
0 Maoni