TANGAZA HAPA

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan anusurika kifo

Aliekuwa Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan (70)

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan alijeruhiwa katika jaribio la mauaji Alhamisi alipokuwa akiongoza maandamano yake yanayoendelea dhidi ya serikali huko Islamabad.

Kiongozi huyo maarufu wa chama cha upinzani Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) mwenye umri wa miaka 70 alipigwa risasi moja kwenye mguu wake wa kulia, msaidizi wake mkuu Rauf Hassan alithibitishia VOA. Shambulio hilo la bunduki katika mji wa Wazirabad, jimbo la kati la Punjab, lilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 14 kujeruhiwa, akiwemo waziri mkuu huyo wa zamani.

Khan alisafirishwa hadi hospitali ya Lahore, mji mkuu wa Punjab, takriban kilomita 150 kutoka eneo la shambulizi, ambapo madaktari walisema yuko katika hali nzuri, kulingana na msaidizi.

Picha za video zilionyesha mtu mwenye bunduki akimfyatulia risasi kutoka chini Khan ambaye alikuwa juu ya lori lililotengenezwa kwa makusudi ya mkutano akiongoza maandamano hayo.

Chapisha Maoni

0 Maoni