Mwanamke mmoja, Mkazi wa Mlombo katika Halmashauri ya Mji wa Babati, mkoani Manyara, Sophia Bakari (36), amejifungua wodini kwa kusaidiwa na dada yake, baada ya wauguzi wawili waliokuwa zamu Hospitali ya Babati, kugoma kumhudumia wakidai anapaswa kusubiri mpaka wamalize kula.
Sophia anadai alifika hospitalini hapo Disemba 17 mwaka huu, majira ya usiku wa saa 5:00, akiwa amezidiwa na uchungu na alipofika aliwakuta wauguzi wawili, ambao badala ya kumhudumia, walimwambia wanakula, hivyo atangulie wodini mwenyewe akachague kitanda.
Akielezea mkasa huo mwanamke huyo, alisema huduma aliyotarajia kupatiwa na wauguzi wa zamu siku hiyo hakupatiwa kama inavyotakiwa, huku akiiomba Wizara ya Afya na Mkuu wa Mkoa huo, Makongoro Nyerere, kufuatilia tukio hilo na kuwawajibisha wauguzi hao.
CHANZO: NIPASHE
0 Maoni