TANGAZA HAPA

Burkina Faso yamtaka mkuu wa Umoja wa Mataifa kuondoka mara moja

Barbara Manzi

Burkina Faso imemuamuru afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kuondoka mara moja.

Serikali ya kijeshi ilimtangaza mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Barbara Manzi kama ‘’mtu asiyekubalika’’.

Waziri wa Mambo ya Nje Olivia Rouamba alisema matamshi ya hivi majuzi ya onyo rasmi la Umoja wa Mataifa kuhusu machafuko yanayokuja yanayosababishwa na waasi wa Kiislamu yameidharau Burkina Faso na kuwaweka mbali wawekezaji.

Makundi ya waasi yamesababisha karibu watu milioni mbili kutoroka makazi yao na kusababisha mapinduzi mawili ya kijeshi ndani ya mwaka mmoja.

Wengi wa waliotoroka makazi yao wanaishi katika kambi zinazosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Chapisha Maoni

0 Maoni