Mahakama ya Wilaya Mpanda mkoani Katavi imemuhukumu Seif Salumu (22) kifungo cha miaka 30 Jela baada ya kukutwa na kosa la kumbaka mtoto (11) kwa nyakati tofauti.
Akisoma hukumu hiyo jana Desemba 6, 2022 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya Mpanda Rebecca Mwalusako, amesema mtuhumiwa alitenda kosa hilo kuanzia Septemba 1,2022 hadi 17 kwa nyakati tofauti.
Amesema mtuhumiwa walikua majirani na familia ya mtoto huyo hivyo alikua akimuagiza kwenda kuiba hela nyumbani kwao nakisha kuzipeleka kwake ili aendelee kumfanyia ukatili huo.
Mtoto huyo alipohojiwa na Mahakama alisema Sefu amekua akimfanyia hivyo mara kwa mara baada ya kumpa hela hizo alikua akimlaza kwenye godoro lililokua chini na kumfanyia ukatili huo.
Mama wa mtoto baada ya kuulizwa mahakamani hapo amesema aligundua mtoto wake anafanyiwa ukatili huo baada ya pesa kupotea ndani ndipo alipowaita watoto wote kuwauliza aliechukua pesa hiyo baada ya vitisho vingi mtoto huyo alikiri kuchukua pesa hiyo huku akidai amekua akitumwa na mtuhumiwa.
Hata hivyo Shahidi wa tatu wa kesi hiyo kutoka upande wa mashitaka ambae ni daktari kutoka Hospital ya Rufaa Mkoa wa Katavi ameiambia mahakama kuwa alimpokea mama huyo akiwa na mtoto wake na baada ya kufanya uchunguzi alibaini kuwa mtoto huyo aliingiliwa.
Wakili shayo amesema mbali na hukumu hiyo pia mahakama ilimuamuru mtuhumiwa kumlipa kiasi cha shilingi milioni moja muhanga wa tukio hilo.
Hatahivyo mtuhumiwa baada ya kupewa nafasi ya kujitetea alikana kutenda kosa hilo huku akidai amesingiziwa kutokana na ugomvi wa muda mrefu wa kibiashara uliopo baina yake na mama wa mtoto huyo.
0 Maoni