TANGAZA HAPA

Shinyanga; Bibi auawa kwa kukatwa mapanga


Bibi aliyefahamika kwa jina la Mbalu Shija (68) mkazi wa kijiji cha Mwalukwa wilayani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa mapanga kichwani na ubongo kutoka nje akidaiwa ni mshirikina.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7 usiku akiwa amelala nyumbani kwake.

Mwenyekiti wa kijiji Mwalukwa Lucas Buchambi akisimulia tukio hilo leo, amesema Bibi huyo hua ana kaa na wajukuu zake, lakini usiku huo hawakuwepo walikuwa kwa jirani wakijiandaa maandalizi ya kuimba kwaya kwenye mkesha wa siku sikuu ya Christimas.

Amesema wajukuu zake waliporudi nyumbani usiku huo, ambapo mmoja hua analala na bibi yake alipoingia chumbani akamuona bibi yao ameanguka chini akiwa ameuawa, ndipo akapiga kelele kuomba msaada.

"Baada ya kupata taarifa za tukio hili majira ya saa 8 usiku niliamka nikaenda eneo la tukio na kumkuta bibi huyu akiwa ameuawa vibaya kwa kukatwa mapanga kichwani huku ubongo ukiwa nje," amesema Buchambi.

"Chanzo za tukio hili ni imani za kishirikina, marehemu alikuwa akituhumiwa kuwa ni mchawi,na mhusika ambaye ana tuhumiwa kutekeleza mauaji haya tayari ameshakamatwa na Jeshi la Polisi,"ameongeza.

Naye Kaimu Mtendaji wa Kata ya Mwalukwa Elipendo John, amelaani tukio hilo la kimyama na kueleza kuwa matukio ya mauaji ya mapanga kwa wazee yalikuwa yameisha Shinyanga, lakini anasikitika kuanza kuibuka upya na kupinga vikali mauaji hayo.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa Jeshi linaendelea na uchunguzi zaidi.

Chapisha Maoni

0 Maoni