TANGAZA HAPA

Jela kwa kumbaka mtoto wa mke wake


Mahakama ya wilaya Manyoni mkoani Singida imemhukumu kijana Sanya Kalamangola mwenye umri wa miaka 25 kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kumbaka mtoto wa mke wake mara baada ya mkewe kwenda kumuuguza mjamzito.

Akisoma shauri hilo la jinai namba 36 ya mwaka 2023 baada ya upelelezi kukamilika Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri Ryoba Mkambala, ameiambia mahakama kuwa mnamo tarehe 2/05/2023 mshtakiwa huyo Sanya Kalamangola, maarufu kwa jina la Bakari alitenda kosa hilo muda wa usiku wakati mama mzazi wa binti huyo akiwa ameenda kumuuguza mzazi kijiji hapo.

Mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la kumbaka binti wa miaka 14 ambaye walikuwa wakiishi pamoja na mama yake mzazi, huku akijua kufanya hivyo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 130 (1) na (2) e na 131 (1) sura ya 16 ya kanuni ya adhabu iliyofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Baada ya upelelezi wa shauri hilo kutolewa na mahakamani na kujiridhisha Mwendesha Mashataka akaiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa mshatikwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kufanya ukatili wa aina hiyo

Hakimu Mkazi Simon Kayinga, baada ya kujiridhisha na mwenendo wa kesi hiyo na ushahidi uliotolewa ikamtia hatiani pasi na shaka kwa kumhukumu Sanya kwenda jela miaka 30.

Chapisha Maoni

0 Maoni