TANGAZA HAPA

Jela maisha kwa kumbaka mtoto wa dada yake

mtyzonline255.com

Mahakama ya Wilaya ya Iringa, imemuhukumu kifungo cha maisha jela na kulipa fidia ya Tsh. Milioni tano Joshua Mkwalakwala (35) Mkazi wa kijiji cha Makota mkoani Iringa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka 10 aliyekuwa akisoma darasa la nne.

Tukio hili lilitokea Agosti 22 mwaka jana majira ya saa 9 mchana ambapo siku ya kwanza Joshua alianza kwa kumuonesha Mtoto huyo sehemu zake za siri (uume) akimwambia "Unaijua hii?" ndipo Mtoto huyo akakimbia, siku ya pili alimfuata Mtoto huyo akiwa na anacheza na wenzake na kumpeleka vichakani kisha kumfanyia kitendo hicho.

Kesi hii ilikuwa na jumla ya Mashahidi watano ikiongozwa na Waendesha mashtaka wawili Nashoni Saimon pamoja na Baton Mayage, akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mahakama imemkuta na hatia baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka, Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba Mahakama imuonee huruma na imuachie huru ili aweze kulipa fidia.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni