Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, imeyafutia ratiba za kusafiri mabasi tisa yaendayo mikoani kwa kosa la kwenda mwendokasi na kuhatarisha maisha ya abiria, kwa kuzingatia kanuni ya 27(2) ya kanuni ya leseni za usafirishaji magari ya abiria.
Kwa mujibu wa taarifa ya LATRA, imeeleza kuwa mabasi hayo sasa yataanza safari zake kuanzia Jumatano, Juni 21, 2023 saa 12:00 asubuhi na endapo maelekezo hayo yatakiukwa au kutozingatiwa basi mabasi hayo yatafutiwa leseni.
aarifa hiyo imeyataja mabasi hayo kuwa ni tisa yanayoanza safari zao kuanzia saa 9:00 alfajiri ambayo ni ni sita ya Ally’s Star (T946 EBF, T947 EBF, T948 EBF , T354 DXS, T357 DXS na T360 DXS) na matatu ya Katarama Express (T835 EBR, T836 EBR na T212 ECR).
Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Mabasi hayo yamepewa adhabu hiyo kutokana na kuendelea kukiuka sheria, kanuni na taratibu hata baada ya kupatiwa elimu na maonyo mara kadhaa ambayo wamekuwa wakipatiwa na vyombo vya usalama ikiwemo LATRA.
0 Maoni