Waziri mkuu Kassim Majaliwa |
Serikali imeondoa rasmi katazo la mabasi kusafiri usiku kufuatia mabadiliko chanya na maoni ya wadau.
Hilo ni miongoni mwa maagizo yanayohitaji utekelezaji yaliyotolewa jana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alipokuwa akiahirisha Bunge jijini Dodoma.
Waziri Majaliwa alitangaza rasmi kuanza kwa safari hizo usiku kwa sharti la wamiliki kuomba vibali vya kufanya hivyo.
Wakati akitangaza hatua hiyo bungeni, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema zuio hilo liliwekwa mwaka 1992 kufuatia kuongezeka kwa ajali za barabarani na utekaji wa mabasi.
Sasa ameziagiza mamlaka husika kufanya kazi ya “kuweka utaratibu utakaofuatwa na wamiliki na madereva wa mabasi ya abiria wanaokusudia kusafirisha abiria usiku”.
0 Maoni