Mahakama Kuu Kanda ya Tanga imewahuku watu 10 hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji la aliekuwa mlinzi wa ofisi ya kijiji cha Lulago wilaya ya kilindi mkoa wa Tanga.
Hukumu hiyo iliyosomwa na jaji mfawidhi kanda ya Tanga Latipha Mansoor amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahaka imejiridhisha na kuwatia hatiani watuhumiwa hao.
Awali washtakiwa hao walikuwa 20 ambapo washtakiwa wa kosa la ugaidi huku tisa (9) kati yao wakiachiwa huru baada ya mahakama kukosa ushahidi mwaka 2022 na baadae mashtaka yakabadilishwa na kuwa kesi ya mauaji.
Waliohukumiwa ni Haji Omary Mzana, Khalid Salehe Sekinzu, Omary Said, Abdulrahman Hassan, Juma Omary, Ramadhani Athumani Mnguu na Jawa Omari Mzana huku mshtakiwa mmoja akiachiwa huru baada ya upande wa ushahidi kuonyesha kuwa ameshtakiwa kwa jina lisilokuwa la kwake.
0 Maoni