TANGAZA HAPA

Watoto wampiga mama yao baada ya kuolewa na mwanaume mwengine


KENYA; Mama mmoja kutoka nchini Kenya amepigwa na watoto wake waliopandwa na hasira walipoona amemuacha baba yao na amekwenda kuolewa na mwanaume mwingine.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tuko ya nchini humo wamepigwa yeye na mume wake ambao kwa sasa wanauguza majeraha wote.

Inadaiwa wanandoa hao kutoka kaunti ya Samburu walivamiwa na watoto waliokuwa na silaha na kumuacha baba yao huyo wa kambo akiwa kipofu kutokana na kumtoboa macho.

"Niliaibika, walivamia nyumba yetu na kuanza kunipiga kisha wakamwendea mume wangu baada ya kumkuta ndani ya nyumba hiyo, wakamvamia machoni mwake," amesema mama huyo aliyetambulika kwa jina la Sylevena.

"Walikuwa na silaha kama vile rungu na panga. Walimkata mke wangu kichwani na mimi machoni," kwa masikitiko Elisha ambaye ndiye mume mpya wa Sylevena alisema.

Chapisha Maoni

0 Maoni