TANGAZA HAPA

Watu 11 Kizimbani kwa kusafirisha meno ya tembo na kucha za simba


Watu 11 wakiwemo wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka 11 likiwemo la kusafirisha meno na kucha za simba.

Aidha watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi vibali vya kusafirisha samaki aina ya kaa na kutakatisha fedha kiasi cha Sh. Bilioni 3.2.

Wakisomewa mashtaka yao Jana Juni 16, 2023 na jopo la mawakili watatu wa serikali wakiongozwa na Faraja Ngukah, Neema Moshi na Eric Davies mbele ya Hakimu Mkazi Rhoda Ngimilanga imedaiwa kuwa walikuwa wakizisafirisha nyara hizo kutoka Tanzania na Msumbiji kuzipeleka Malaysia.

Wakili Ngukah amedai kuwa washtakiwa hao walikuwa wakizisafirisha nyara hizo bila kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyama Pori.

Chapisha Maoni

0 Maoni