Kijana mmoja katika jimbo la Iowa nchini Marekani ambaye alimpiga mwalimu wake hadi kumuua kwa fimbo kutokana na matokeo mabaya shuleni amehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Willard Miller, 17, alikiri kosa la mauaji ya daraja la kwanza mwezi Aprili kwa jukumu lake katika mauaji ya Nohema Graber, mwalimu wa Uhispania tarehe 2 Novemba 2021.
Miller na mshtakiwa mwenzake Jeremy Goodale, ambaye sasa ana umri wa miaka 18, walimshambulia Bi Graber, 66, baada ya kusahihisha kazi ya Miller.
Wakiwa na umri wa miaka 16 wakati wa mauaji hayo, wote wawili walishtakiwa wakiwa watu wazima.
Hukumu ya Goodale imepangwa Agosti.
Siku ya Alhamisi, Miller alihukumiwa kifungo cha maisha jela na uwezekano wa kupewa kifungo cha nje tu baada ya angalau miaka 35.
Pia aliamriwa kulipa angalau $150,000 (£117,000) kwa familia ya mwathiriwa.
Kabla ya kutoa hukumu yake, Jaji Shawn Showers alikataa hoja za utetezi kwamba Miller alikuwa mdogo sana wakati huo kuelewa uzito wa matendo yake.
“Uovu hauna siku ya kuzaliwa,” alisema.
Wanafamilia wa Bi Graber waliambia mahakama kuwa hawakuamini kwamba Miller alikuwa akijutia alichotenda.
0 Maoni