UGANDA; Kundi la waumini wa Kanisa la Bungonya lililoko wilayani Kayunga nchini Uganda, wamesusia shughuli za ibada baada ya watu wawili kufumwa wakifanya mapenzi ndani ya kanisani hilo.
Jumanne Julai 5, 2023, saa 2 usiku, mwanaume huyo (23), anayedaiwa kuwa mwanandoa na baba wa watoto wawili, alifumwa na mwanamke ambaye alitalakiwa na mumewe siku chache zilizopita na kulazimika kuishi kwa bibi yake katika kijiji hicho.
Tukio hilo la kushtusha, liliibuliwa na mke wa ndoa wa mwanaume huyo ambaye baada ya kumkuta mumewe akifanya mapenzi ndani ya kanisa alipiga kelele iliyowafanya waumini kujaa na kuwakamata watu hao wakiwa utupu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bungonya lilipotokea tukio hilo, George William Kanda amesema watu hao waliingia kanisani kupitia dirishani kabla ya kuanza kufanya tukio hilo.
"Waliingia kanisani kupitia dirishani kwa sababu mlango ulikuwa umefungwa," amesema.
"Mke wa ndoa wa mwanaume huyo alipowafumania alipiga kelele, watu wakajaa kanisani na kuwakamata kisha kuwaleta ofisini kwangu. Mtandio wa kichwani na fulana (t-shirt) ya mwanaume vimehifadhiwa kwa mwenyekiti kama udhibitisho," amesema Kanda.
0 Maoni