Watu wanne wa familia moja akiwemo mtoto wa miaka 5 wamefariki dunia baada ya gari aina ya fuso kugonga pikipiki iliyobeba abiria watatu wilayani Masasi mkoani Mtwara.
Ajali hiyo imetokea Julai 2, 2023 saa 1:30 usiku eneo la Napupa barabara ya Masasi-Newala wilayani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kubainisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutochukua tahadhari wakati anajaribu kulipita gari lingine.
Amefafanua kuwa gari hilo Mitsubishi Fuso iliyokuwa ikiendeshwa na Shaban Hashim (37) iliigonga pikipiki iliyokuwa ikiendeshwa na Danford Milanzi (29) na kusabisha kifo chake na abiria watatu.
Amewataja wengine waliofariki kwenye ajali hiyo kuwa ni Omega Danford (27) Mosses Danford (5) na Norah Mpili (25).
Amesema miili ya marehemu hao ilifanyiwa uchunguzi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Masasi na kukabidhiwa kwa ndugu.
0 Maoni