TANGAZA HAPA

Tetesi za Soka Ulaya 03.01.2024


Uhamisho wa kiungo wa kati wa Manchester City na England Kalvin Phillips, 28, kwenda Newcastle United unaweza usifanyike. Lakini Fulham na Crystal Palace wanavutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Leeds. (I Sport)

Manchester United wameandaa orodha ya wachezaji wanne ili kupata mshambuliaji mpya mwezi Januari, nao ni Mcameroon wa Bayern Munich, Eric Maxim Choupo-Moting, 34, mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller, 34. Klabu hiyo pia imewasiliana na RB Leipzig juu ya Timo Werner wa Ujerumani, 27, na mshambuliaji wa Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy, ​​27. (Athletic)

Mshambulizi wa Uingereza, Ivan Toney, 27, ana matumaini ya kuhamia Arsenal mwezi Januari lakini The Gunners hawana nia ya kulipa pauni milioni 100 ambayo Brentford wanataka. (Football Transfers)

Winga wa Manchester United na England, Jadon Sancho, 23, anatamani kurejea Borussia Dortmund. (Fabrizio Romano)

Tottenham hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza, Conor Gallagher, 23, mwezi Januari kwa sababu hawawezi kutimiza matakwa ya Chelsea ya pauni milioni 60 kutokana na vikwazo vya kifedha (Football Transfers)

Everton wanafikiria kumpa kiungo wa zamani wa Manchester United na Uingereza Jesse Lingard mkataba hadi mwisho wa msimu huu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kwa sasa ni mchezaji huru. (Talksport)


Mshambulizi wa Aston Villa na Colombia Jhon Duran, 20, analengwa na AC Milan ya Italia. (Sky Sports)

Mlinzi wa West Ham na Jamhuri ya Czech, Vladimir Coufal, 31, hajafurahishwa na mkataba wake na anataka klabu hiyo imwache ondoke katika dirisha la uhamisho la Januari ikiwa hatopewa mkataba mzuri. (Sky Sports)

Arsenal wameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya kwa mlinzi wao raia wa Japan, Takehiro Tomiyasu, 25. (Mail)

The Hammers wanataka kufufua mpango wao kumnunua mlinzi wa Wolves na England, Max Kilman, 26. (Talksport)

Mshambulizi wa Wolves na Austria, Sasa Kalajdzic, 26, analengwa na Eintracht Frankfurt, huku klabu hiyo ya Ujerumani ikisubiri kuona kama Gary O'Neill ataidhinisha uhamisho wa mkopo. (Mail)

Mpango wa Fulham kumnunua kiungo wa kati wa Fluminense na Brazil, Andre, 22, umesitishwa kwa sababu hawataki kufikia bei inayotakiwa ya pauni milioni 25. Na sasa wanaamini kiungo wa kati wa Ureno, Joao Palhinha, 28, atasalia katika klabu hiyo. (Football Transfers)

Liverpool hawana nia ya kuwasajili Palhinha Gonçalves, André Trindade da Costa Neot na mlinzi wa Bayer Leverkusen na Ecuador, Piero Hincapie, 21, wakati wa dirisha la usajili la Januari. (Ben Jacobs)


Winga anayecheza kwa mkopo Everton, Arnaut Danjuma, 26, analengwa na Lyon. (Mail)

Brentford wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji wa Real Betis mwenye umri wa miaka 18 na mshambuliaji wa Uhispania, Assane Diao kuhusu mkataba wa Januari. (Football Transfers)

Borussia Dortmund wamefanya mazungumzo na beki wa Chelsea Mholanzi, Ian Maatsen, 21, kuhusu uhamisho wa Januari lakini The Blues wanashikilia dau la pauni milioni 30. (The Standard)

Mpango wa Crystal Palace wa kumnunua beki wa Peterborough na England, Ronnie Edwards, 20, umekataliwa. Wanakabiliwa na ushindani kutoka vilabu vitano vya Ligi Kuu ya Uingereza. (Talksport)

Klabu ya Italia, Atalanta inakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Birmingham City na Wales, Jordan James, 19, baada ya kutuma ofa ya pauni milioni 3.9. (Tuttomercato)


Chapisha Maoni

0 Maoni